Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga
(IGUWASA)

Miradi Inayoendelea

Mradi wa ukarabati wa Mfumo wa Uzalishaji wa Maji katika chanzo cha bwawa la Bulenya na ujenzi wa mtandao wa kusafirisha maji safi kutoka katika mfumo wa kusafisha maji uliopo Igogo hadi kwenye tanki kuu la Mwamaganga.

Malengo ya Mradi: Kuboresha utoaji wa maji safi na salama.

Tarehe ya Kuanza kwa Mradi: Mradi ulianza Aprili 29, 2025.

Tarehe ya Kukamilika kwa Mradi: Mradi utakamilika Aprili 17, 2026.

Gharama za Mradi: Mradi huu umegharimu jumla ya TZS: 3,477,478,945.00.

Mbinu ya Utekelezaji wa Mradi: Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi PNR SERVICE LTD.

Kazi za Kutekelezwa:

1. Ukarabati wa chujio la maji lililopo - Igogo.

2. Ujenzi wa mfumo mpya wa kusafirisha maji ghafi kutoka Bwawa hadi Igogo - WTP.

3. Ujenzi wa mtandao wa kusafisha maji wa kipenyo cha mm 250 kutoka Igogo WTP hadi Tangi la Mwamaganga.

4. Ujenzi wa Pampu House ikiwa ni pamoja na ununuzi wa pampu mbili mpya.

5. Ukarabati wa nyumba za huduma zilizopo - Igogo WTP.

Kazi Zilizotekelezwa:

1. Maandalizi ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kambi itakayotumiwa na mkandarasi.

2. Uhamasishaji wa wafanyakazi muhimu.