Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga
(IGUWASA)

Miradi ambayo Imekamilika

Upanuzi wa Mtandao wa Mtandao wa Majisafi na Salama kutoka Makomero mpaka Mgongoro.

Lengo la Mradi: Kuboresha huduma ya Majisafi na Salama

Tarehe ya Mradi kuanza: Mradi ulianza tarehe 17 Septemba, 2024.

Tarehe ya Mradi Kumalizika: Mradi utakamilika 17 Mei, 2025.

Gharama ya Mrad: Mradi huu umegharimu jumla ya kiasi cha TZS: 840,877,205.00.

Njia ya utekelezaji wa Mradi: Mradi huu unatekelezwa kwa utaratibu wa Force Account, Chini ya usimamizi wa IGUWASA.

Kazi Zitakazotekelezwa: 

1. Uchimbaji na Ufukiaji wa Mtaro wenye urefu wa kilomita 25.

2. Kubeba, Kuunga na kulaza bomba za HDPE 110mm, HDPE 90mm & HDPE 63mm zenye urefu wa kilomita 25.

3. Ujenzi wa vituo vipya sita vya kuchotea Maji.

4. Ukarabati wa vituo sita vya kuchotea maji pamoja na kuviunganisha na huduma ya Majisafi na Salama.

5. Kuunganisha huduma ya Maji katika manywesheo mawili ya mifugo.

Kazi Zilizotekelezwa: 

1. Uchimbaji na ufukiaji wa Mtaro wenye urefu wa kilomita 25.

2. Kunga na Kulaza bomba zenye urefu wa kilomita 25

3.  Ujenzi wa vituo 6 vipya, ukarabati wa vituo 6 vya zamani na manywesheo mawili pamajo na kuunganisha huduma ya maji.

4. Ujenzi wa chamber 9Nos za valve.

5. Uzinduzi wa mradi uliofanyika tarehe 31/7/2025 na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2025.