Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga
(IGUWASA)

Historia na Kazi za Msingi

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Igunga (IGUWASA) ni Taasisi ya Serikali yenye jukumu la kutoa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa wananchi wa mjini Igunga. IGUWASA ilianzishwa na Waziri mwenye dhamana ya maji tarehe 24 Disemba, 1999 na kutangazwa rasmi na Gazeti la Serikali tarehe 31 Disemba, 1999 kupitia GN Na. 451. Hii ni kutokana na sheria iliyokuwepo Na. 8 ya mwaka 1997 na kwa sasa inatambulika kwa Sheria Na.5 ya mwaka 2019. Mamlaka ilianza kufanya kazi zake rasmi Februari 2000.

MAJUKUMU YA IGUWASA.

 a) Kuhakikisha Mamlaka inatoa huduma ya Majisafi na salama yanayotosheleza mahitaji kulingana na viwango vya ubora wa Maji vilivyotolewa.

b) Kupanga bei za Maji ambazo zitaiwezesha Mamlaka kuendelea kutoa huduma ya Maji bila kuathiri kundi lolote la watumiaji.

 c) Kuendelea kutunza vyanzo vya Maji na matumizi bora ya Maji.

 d) Kupanga na kutekeleza Miradi Mipya ya Maji.

e) Kukusanya maduhuli kutoka kwa watumiaji wa Maji na kuyatumia kwenye kuendesha shughuli za Mamlaka.

 f) Kutunza Mazingira katika eneo ambalo Mamlaka ya Maji inahudumia ili kusitokee uchafuzi.

g) Kutoa taarifa Serikali kuu kuhusu shughuli zote kubwa ambazo zinazoweza kuathiri utoaji wa huduma ya Maji.

 h) Kuhudhuria kikamilifu katika Mikutano yote itakayoandaliwa na serikali katika maeneo yatakayotajwa.

 i) Kuandaa na kutoa taarifa za kila Robo, Mwaka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, EWURA na kwa Mkurugenzi wa Wilaya.